Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Frequently Asked Questions

Je Tanzania imewaandaaje wananchi kwenye suala la umiliki wa Ardhi
Answer:

Suala la Ardhi litaendelea kuongozwa na sera na sheria za Nchi Wanachama. Aidha Serikali inaendelea na taratibu za kupitia sheria na kanuni, maandalizi ya kupanga matumizi ya ardhi, kupima ardhi na kumilikisha ardhi kwa wananchi.

   Read More
Je tumejiandaa vipi katika suala la elimu?
Answer:

Tanzania imeweka mikakati madhubuti katika suala zima la kuboresha elimu kwa kutoa elimu bora na ya kiwango kuanzia shule za awali hadi vyuoni.

   Read More
Mbona lugha yetu ni tatizo, nchi yetu wanaon- gea Kiswahili
Answer:

Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki unakithamini Kiswahili na unakitambua kama lugha ya mawasiliano ndani ya Jumuiya. Aidha, katika kuhakikisha kuwa kiswahili kinaendelezwa maandalizi ya kuanzisha Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaendelea

   Read More
Je hatua gani zinachukuliwa na Wizara ili kuondoa hofu ya wananchi kuhusu Afrika Mashariki?
Answer:

Kama wizara tunatekeleza programu mbalimbali za kuwaelimisha wananchi kuhusu Jumuiya kwa njia ya redio, luninga, magazeti, mihadhara, makongamano, tovuti, machapisho.

   Read More
Bidhaa za Rwanda na Burundi zinatozwa ushuru kiasi gani?
Answer:

Bidhaa za Rwanda na Burundi hutozwa ushuru wa asilimia 20 tu hii ni baada ya makubaliano kwamba Rwanda na Burundi hazitozwi ushuru katika biashara kati yake na Kenya na zimepunguza ushuru kwa asilimia 80 kwa bidhaa zitokazo Uganda.

   Read More
Je inakuwaje kunakuwa na Wizara ya Ushiriki- ano wa Afrika Mashariki wakati tulikataa wazo la Afrika Mashariki wakati wa kukusanya maoni mwaka jana?
Answer:

Kilichokataliwa na wananchi mwaka 2007 ni kuharakishwa kwa Shirikisho la Kisiasa ambapo wananchi walitaka twende kwa utaratibu uliokubaliwa katka Mkataba ambao ni wa hatua kwa hatua, tukianza na hatua ya Umoja wa Forodha ikifuatiwa na Soko la Pamoja na kisha Sarafu moja na hatimaye Shirikisho la

   Read More
Kuna uhusiano gani kati ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa?
Answer:

Wizara hizi zinahusika na mahusiano ya Tanzania na nchi za nje, ila Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inasimamia na kuratibu uendelezaji wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

   Read More