Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Frequently Asked Questions

Kwa kuwa Kenya ina Uchumi ulio imara zaidi kuliko Nchi nyingine Wanachama hamuoni kuwa Nchi kama Tanzania itakuwa tu Soko la Bidhaa za Kenya
Answer:

Tanzania imepewa muda wa kujiandaa kwani ilionekana kuna bidhaa kutoka Kenya zikiingia nchini bila kutozwa ushuru zinaweza kuathiri viwanda vyetu.

   Read More
Kuna hatua gani zinachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wanyonyao kama kutoka Kenya?
Answer:

Ipo kamati ya kitaifa ambayo hushughulikia vikwazo vya kibiashara (Non- Tariff Barriers) katika Nchi wanachama wa Jumuiya inayokutanisha wadau kutoka Sekta ya Umma na Sekta binafsi. Hivyo yeyote mwenye malalamiko katika biashara anaombwa kutoa taarifa katika Kamati hiyo au katika Wizara.

   Read More
Pamoja na manufaa, nini changamoto katika hii Jumuiya?
Answer:

Changamoto kubwa ni jinsi ya kuwaandaa watanzania ili waweze kuendana na kasi kubwa ya mtangamano wa Jumuiya inayoendelea, uchanga na utegemezi wa Sekta Binafsi kwa Serikali, kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa kukidhi mahitaji ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, miundombinu duni, matumizi

   Read More
Kuna mafanikio gani ya Tanzania kuwa ndani ya Jumuiya mpaka hivi sasa?
Answer:

Tangu mwaka 2005 mafanikio yaliyopatikana ni yale yatokanayo na utekelezwaji wa hatua ya Umoja wa Forodha, kuimarika kwa biashara baina ya nchi wanachama, Mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Afrika Mashariki yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.

   Read More
Nchi ya Kenya ina bidhaa nyingi za viwanda, je, Tanzania inauza nini katika soko la Kenya?
Answer:

Bidhaa ambazo Tanzania inauza kwa wingi katika nchi za Afrika Mashariki ni pamoja na bidhaa za chumvi, umeme na vifaa vya umeme, mafuta ya kupikia, chuma, magunia, nafaka,
sabuni, nyama , vifaa vya plastiki, kahawa iliyosindikwa na nondo

   Read More
Mtu wa hali ya chini na wa kawaida atanufaika vipi na hii Jumuiya?
Answer:

Dira kuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kukuza kipato, kuinua hali ya maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki, kukuza uchumi, na kujenga ushindani wa kanda katika ngazi ya kimataifa. Katika kutekeleza azma hii, Nchi Wanachama zinanufaika kutokana na mahusiano mazuri ya kibiashara na uwekezaji.

   Read More
Ni lini mtaondoa visa za wanafunzi
Answer:

Ndani ya nchi yoyote ya Jumuiya, wanafunzi au mtu yoyote yule hawatakiwi kuwa na viza.

   Read More
Je kuna pasi ya kusafiria inatakiwa nikitaka kwenda Rwanda au Uganda?
Answer:

Unapokwenda kwenye nchi yoyote mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unalazimika kutumia pasi ya kusafiria ya nchi yako au pasi ya kusafiria ya Jumuiya.

   Read More
Kwanini mmeziingiza nchi za Rwanda na Burundi na kuziita za Afrika mashariki wakati nchi hizo kijiografia ziko Afrika ya Kati?
Answer:

Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaruhusu nchi yoyote itakayoomba uana-
chama kujiunga, ili mradi itimize masharti na
vigezo vilivyowekwa.

   Read More
Tuna uhakika Rwanda na Burundi wameacha vita? kwanini wamekubaliwa?
Answer:

Vigezo mbalimbali vimewekwa ambavyo hutumika kabla ya kuwakubali kuwa wanachama katika Jumuiya. Vigezo hivyo ni pamoja na kudumisha amani na utawala bora. Nchi hizo zilikubaliwa baada ya kukidhi masharti na vigezo hivyo.

   Read More