Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA TAREHE 5-15 OKTOBA 2015

MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA LEO

Mkutano wa pili, kipindi cha nne wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaanza leo tarehe 5 Oktoba, 2015 Jijini Nairobi, Nchini Kenya, katika ukumbi wa Bunge la Nchi hiyo. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika kwa siku 11, kuanzia tarehe 5 hadi 15 Oktoba 2015.

Mkutano huu unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta siku ya jumanne tarehe 6 Oktoba, 2015.

Katika Mkutano huu, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) pamoja na mambo mengine litatumia vikao vyake kupokea na kujadili ripoti za kamati mbalimbali za Bunge na kujadili miswada mitatu ya kisheria. Miswada hiyo  itakayo jadiliwa ni;

  • Muswada wa sheria wa miamala ya elektoniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2014 (The EAC Electronic Transaction Bill 2014).
  • Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kusimamia na kulinda Misitu wa Mwaka 2015 (The EAC Forests Management and Protection Bill 2015).
  • Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kupunguza na kukabiliana na majanga (The East African Community Disaster Risk Reduction and Management Bill)

Katika Mkutano huu wa pili wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo tarehe 12 Octoba, 2015 na atatumia fursa hii kuliaga Bunge hilo.

 

Imetolewa na, 

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Event Date: 
Monday, October 5, 2015 - 08:30 to Thursday, October 15, 2015 - 16:15